Meagan Good na Jonathan Majors ni wachumba

Marion Bosire
1 Min Read

Waigizaji Jonathan Majors na Meagan Good sasa ni wachumba.

Walifichua hayo kwenye hafla ya Ebony Power 100 huko Los Angeles ambapo Good alionyesha pete ya uchumba akipigwa picha.

Majors wa umri wa miaka 35 na Good wa miaka 43, walikutana mwaka 2022 lakini mahusiano yalianza rasmi mwaka jana.

Meagan alikuwa mmoja wa watu ambao walikuwa wakiandamana na Majors kwa kesi ya kumdhulumu mpenzi wake wa awali huko New York.

Majors aliamuriwa kukamilisha mpango wa ushauri nasaha wa mwaka mmoja lakini hakuhukumiwa kifungo gerezani kwa sababu alikuwa mkosaji wa mara ya kwanza.

Hata hivyo yeye na mawakili wake wanasisitiza kwamba hakufanya kosa hilo.

Kesi hiyo hata hivyo iliathiri kazi yake kama mwigizaji kwani aliondolewa kwenye kazi kadhaa za kampuni ya Marvel.

Anaigiza kwenye filamu ya “Magazine Dreams” kama mtu anayetaka kuwa mjenga misuli kupitia mazoezi, kazi inayotarajiwa kuzinduliwa mwaka ujao.

Good naye ameigiza kwenye filamu kama “Eve’s Bayou”, “Deliver Us From Eva” na “Roll Bounce” na kipindi cha kampuni ya Nickelodeon kiitwacho “Cousin Skeeter”.

Website |  + posts
Share This Article