Mchungaji Ezekiel ashindwa rufaa ya kufungwa kwa kanisa la Kilifi

Dismas Otuke
1 Min Read

Mahakama ya Rufaa jana Jumatano ilitupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na Mchungaji Ezekiel Odero kupinga kupokonywa leseni ya kanisa lake la Kilifi.

Mchungaji Odero alikuwa amewasilisha rufaa kupinga uamuzi wa mahakama kuu kumpokonya leseni ya kanisa la New Life  Prayer Centre and Church tawi la Kilifi kwa kushindwa kuthibitisha kulipa ushuru.

Kulingana na majaji watatu waliokuwa wakiskiza kesi hiyo, Odero alishindwa kutumia mbinu mbadala ya kutatua mizozo kabla  ya kuelekea mahakamani.

Majaji Daniel Musinga, Kathurima M’Inoti na Mwaniki Gachoka walisema badala ya Odero kukata rufaa kwa Wizara ya Usalama wa Taifa kupinga kupokonywa leseni, aliwasilisha kesi mahakamani.

Kanisa hilo lilipokonywa leseni Mei 18 mwaka uliopita na msajili wa mashirika baada ya Odero kukosa kulipa ushuru mwaka 2021/2022.

Share This Article