Timu za Kenya za raga ya wachezaji saba kila upande za Shujaa na Kenya Lionesses zimetwaa ubingwa wa makala ya mwaka 2025 ya mashindano ya Safari Sevens.
Shujaa ilitwaa taji ya wanaume baada ya kuwazidia maarifa majirani Uganda pointi 14-10, kwenye fainali ya kukata na shoka iliyopigwa katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.
Lionesses walihifadhi taji ya wanawake baada ya kuwalaza Shogun ya Uhispania alama 14-7, katika fainali.
Makala hayo ya 27 yaliyoanza Ijumaa, yalishirikisha timu 12 za wanaume na 8 za wanawake.