Mbunge wa Kitui Mashariki Nimrod Mbai akamatwa

Marion Bosire
1 Min Read

Mbunge wa Kitui Mashariki Nimrod Mbai amekamatwa na maafisa wa polisi kwa kitendo cha kumzaba kofi afisa wa kampuni ya umeme nchini, KPLC.

Taarifa zinaashiria kwamba Mbai, ambaye alinakiliwa kwenye video akitekeleza kitendo hich, alikamatwa jana Jumanne jioni na atafikishwa mahakamani leo huko Kajiado.

Kwenye video hiyo, Mbai alisikika akiamrisha wafanyakazi wa KPLC wawasiliane na wenzao ambao walikuwa wameng’oa na kuchukua vigingi haramu vya kuunganisha umeme.

Kulingana naye, Rais aliagiza kwamba hali kama hiyo inapotokea, KPLC inafaa kulipisha Wakenya na wala sio kukata umeme.

Afisa huyo wa KPLC anaonekana kusalia mtulivu kwenye video hiyo hata baada ya kuzabwa kofi.

Share This Article
1 Comment
  • Your reporting is fake. Give us the background. The MP has voiced concern over the corruption in the kplc offices. This is just half baked. makes the githeri is innocent media tag stick

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *