Mbunge wa Kilifi Kusini Ken Chong ana spika wa bunge la kaunti hiyo Teddy Mwambire watasalia korokoroni hadi Jumatatu ijayo baada ya hakimu wa mahakama kuahirisha uamuzi kuhusu ombi la kuataka kuachiliwa kwa dhamana.
Wawili hao walikuwa miongoni mwa watu wanne waliokamatwa na polisi Jumatano iliyopita kwa kuhusika katika maandamano ya kupinga serikali eneo la Mtwapa.
Hakimu wa mahakama ya Mombasa Martha Mutuku, alidinda kuwaachilia kwa dhamana Ijumaa akisema ahakuwa amekamilisha kuandika uamuzi wake.