Mshambulizi matata wa Klabu ya PSG na timu taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe, ametangaza kugura uwanja wa Parc des Princes mwishoni mwa musimu.
Haya yanajiri baada yake kukutana na mawakala wa miamba wa Uingereza Manchester City ila hakuweka hadharani waliyojadiliwa.
Hata hivyo, Kwa mujibu wa gazeti la Marca nchini Uhuspani, mfaranza huyo atajiunga na Real Madrid kwa kandarasi ya miaka mitano na atakuwa na mshahara mkubwa wa pauni milioni 17.1 kilabuni humo.
Kiwango hicho kinakaribia nusu ya kile cha pauni million 27.3 anazolipwa kwa sasa pale PSG.
Mshindi huyo wa kombe la dunia mwaka 2018, na mwenye umri wa miaka 25, ana imani kuwa kuondoka huko, kutamwezesha kujiunga na klabu nyingine yenye uwezo mkubwa wa kunyakua kombe la ligi ya ma mabingwa barani Ulaya.
Mbappe alitua Jijini Paris akitokea Monacco Agosti 2017 na amenyakua mataji matano ya ligi kuu ya Ufaransa .