Waziri wa fedha John Mbadi, ametoa ahadi kwamba serikali italipa madeni yote inayodaiwa.
Waziri huyo alidokeza kuwa madeni hayo ambayo ni jumla ya shilingi bilioni 166, yamehujumu uzinduzi wa miradi mipya hasaa katika sekta ya barabara na miundomsingi, ambako zabuni nyingi zimetolewa.
Kulingana na Mbadi, punde tu madeni hayo yatalipwa, serikali itafufua miradi iliyokwama kuhakikisha fedha za serikali zinatumika vilivyo.
Waziri huyo aliyasema hayo katika eneo bunge la Nyatike, akiwa ameandamana na mbunge wa eneo hilo Tom Odege.
Kwa upande wake, Odege ambaye alitoa maoni kuhusu hoja ya kubanduliwa kwa naibu Rais Rigathi Gachagua, alisema uhusiano kati ya rais na naibu wake umehujumu maendeleo ya taifa hili.