Mbadi asema Kenya inatafuta njia zingine za kufadhili bajeti

Martin Mwanje
1 Min Read

Waziri wa Fedha John Mbadi amesema Kenya inatafuta njia zingine mbadala za kufadhili bajeti ya taifa na kulipa madeni. 

Mbadi ameyasema hayo leo Ijumaa alipokutana na Balozi wa Ufaransa humu nchini Arnaud Suquet katika afisini mwake.

Waziri huyo alitoa wito kwa Ufaransa kuisaidia nchi hii katika nyanja kama vile utoaji wa dhamana endelevu (SLBs), Ufutaji wa Madeni na utoaji wa dhamana za mikopo.

Amesema Kenya iko tayari kufanya kazi na Ufaransa.

Nchi hii inakabiliwa na changamoto za ukusanyaji mapato hasa kutokana na kuondolewa kwa Mswada wa Fedha 2024.

Hali hiyo imeilazimu serikali kutafuta njia zingine bunifu za kutafuta fedha kufadhili utekelezaji wa miradi katika sehemu mbalimbali nchini.

Share This Article