Mazishi ya mwanariadha Kevin Kiptum yanaendelea Keiyo Kusini

Tom Mathinji
1 Min Read
Mazishi ya mwanariadha Kevin Kiptum yafanyika Keiyo Kusini.

Ibada ya mazishi ya mwanariadha Kelvin Kiptum, inaendela katika uwanja wa maonyesho wa Chepkorio, Keiyo Kusini. 

Rais William Ruto ni miongoni mwa mamia ya waombolezaji kwenye mazishi hayo.

Rais ameandamana na naibu wake Rigathi Gachagua na mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi.

Waliopo pia kwenye maziko hayo ni waziri wa michezo, Ababu Namwamba miongoni mwa maafisa wengine wakuu serikalini.

Aipowasili, Rais aliwaongoza alioandamana nao kuutazama mwili wa Kiptum kabla ya kutangamana na familia ikiongozwa na babake Samson Cheruiyot,mjane Asenath Rotich na wanawe.

Marehemu atazikwa kwenye shamba alilonunua, ambapo kwa muda wa juma mmoja lililopita, serikali imekuwa ikimjengea nyumba mjane wake.

Nyumba nyingine itajengwa eneo hilo kwa wazazi wake.

Website |  + posts
Share This Article