Mazishi ya hakimu mwandamizi aliyeuawa kwa kupigwa risasi akiwa kazini katika mahakama ya Makadara Monica Kivuti yameandaliwa Machakos.
Kivuti alifariki Jumanne wiki jana akipokea matibabu katika Hospitali ya Nairobi baada ya kupigwa risasi akitoa hukumu .
Mazishi hayo yamehudhuriwa na naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu na maafisa wengine wakuu wa idara ya mahakama nyumbani kwake Yatta kaunti ya Machakos.
Marehemu amemuacha mumewe wakili Mutima Kang’ata, na wanawe Josephine Wanjiru, Michelle Menyi na Elyanna Wanjiru.