May Yul Edochie aingilia muziki

Alitangaza wimbo wake wa kwanza kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Marion Bosire
1 Min Read

May Yul Edochie mke wa kwanza wa mwigizaji wa filamu za Nigeria Yul Edochie ameingilia tasnia ya muziki.

Hii ni baada yake kuzindua wimbo wake wa kwanza kabisa ambao unaitwa ‘Komole’ ambao amehusisha rafiki yake aitwaye Nwando.

Akitangaza kazi hiyo kwenye mitandao ya kijamii, May alielezea kwamba Komole ni neno la ki-Yoruba ambalo linamaanisha kuinama.

Kulingana naye wimbo huo ni wa kuinua nyoyo na kushukuru Mungu kwa kumwezesha pamoja na mashabiki zake kufika mwisho wa mwaka 2024.

Alichapisha bango la wimbo huo ambalo lina picha yake na ya Nwando na kuandika, “Ninafurahia kuwajuza nyote kuhusu wimbo huu wa kuinua nyoyo unapatikana kwenye majukwaa yote.”

May ambaye ana ushawishi mkubwa mitandaoni alipata kujulikana hata zaidi baada ya mume wake Yul Edochie kutambulisha mke wa pili ambaye pia ni mwigizaji kwa jina Judy Austin.

May ambaye pia aliingilia uigizaji hivi maajuzi, alikataa kuhusishwa na ndoa ya wake wengi huku tetesi zikiibuka kwamba tayari ameanzisha mchakato wa talaka.

Aliigiza kwenye filamu ya mchekeshaji na mwigizaji A.Y iitwayo ‘The Waiter’ iliyozinduliwa hivi maajuzi na jana alitangaza kwamba alikuwa amezawadiwa nyumba.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *