Mawaziri wa zamani Ababu Namwamba, Dkt. Andrew Karanja na Dkt. Margaret Ndung’u watafika mbele ya kamati ya Bunge la Kitaifa kusailiwa kwa uteuzi wa kuwa Mabalozi.
Waziri anayeondoka wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali Dkt.. Margaret Ndung’u alitarajiwa kuwa wa kwanza kusailiwa kwa wajibu wake mpya wa Balozi wa Kenya nchini Ghana.
Namwamba aliyekuwa Waziri wa zamani wa Michezo, anasailiwa kwa uteuzi wa Mwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Mataifa katika Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UNEP).
Aliyekuwa Waziri wa Kilimo Dkt. Andrew Karanja anapigwa msasa kwa wadhfa wa Balozi wa Kenya nchini Brazil.
Mwingine atakayepigwa msasa ni aliyekuwa Naibu Inspekta Jenerali Mkuu Noor Gabow aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Kenya nchini Haiti.