Mawaziri waidhinisha ujenzi wa uwanja mpya wa viti elfu 60

Marion Bosire
1 Min Read

Baraza la mawaziri limeidhinisha ujenzi wa uwanja wa michezo wa viti 60,000 utakaotumiwa kuandaa mechi za fainali za komeb la mataifa ya Afrika mwaka 2027 ambazo zitaandaliwa kwa pamoja na mataifa ya Kenya,Uganda na Tanzania.

Baraza la mawaziri limeafikiana siku Jumanne kwenye kikao kilichoongozwa na Rais William Ruto katika kaunti ya Nairobi.

Viwanja vya Moi International Sports Centre-Kasarani, Nyayo na Kipchoge Keino mjini Eldoret, tayari vimeratibiwa kuandaa mechi za kombe la AFCON mwaka 2027.

Kulingana na masharti ya shirikisho la soka Afrika CAF kila nchini ambayo itaandaa fainali za AFCON katika mataifa matatu ya Afrika Mashariki inahitaji kuwa na viwanja viwili vinavyomudu mashabiki zaidi 40,000 na vingine viwili vinavyomudu mashabiki zaidi ya 15,000.

Ivory Coast itaandaa makala ya mwaka ujao ya fainali za AFCON mwaka ujao, kabla ya Morocco kuwa mwenyeji wa kipute cha mwaka 2025 .

Share This Article