Mawakili 242 wafuzu kutoka chuo cha uwakili

Mahafala hao wamehitimu kwenye hafla iliyoongozwa na jaji mkuu Martha Koome katika Mahakama ya Milimani.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mawakili 242 wamefuzu kujumuishwa kwenye dawati la wanasheria baada ya kufuzu kutoka chuo cha uanasheria nchini.

Mahafala hao wamehitimu kwenye hafla iliyoongozwa na jaji mkuu Martha Koome katika Mahakama ya Milimani.

Idadi ya mahafali hao inafikisha jumla ya mawakili waliofuzu mwaka huu kuwa 950.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Koome aliwataka mawakili hao kudunisha kiapo na kutenda kazi kwa kuzingatia sheria zilizopo.

Aidha, Jaji alihoji upungufu wa majaji uliopo nchini huku Majaji 202 pekee wakiwahudumia Wakenya, ikiwa kiwango cha wastani cha jaji mmoja anayehudumia watu 279,000.

 

 

Website |  + posts
Share This Article