Mauritius imefunga mitandao yote ya kijamii nchini humo, hadi Novemba 11,2024 wakati Uchaguzi Mkuu utakapokamilika.
Hatua hiyo ya siku ya Ijumaa ilijiri huku kukiwa na tuhuma za udukuzi, upinzani ukielezea kuhusu njama ya serikali ya kuepuka kushindwa katika Uchaguzi huo.
Halmashauri ya mawasiliano ya taifa hilo, iliagiza kampuni zote za kutoa huduma za mtandao kusitisha upatikanaji wa mitandao ya kijamii hadi Novemba 11,2024.
Kwa mujibu wa afisi ya Waziri Mkuu Pravind Jugnauth, hatua hiyo inalenga kudumisha usalama wa taifa na uadilifu, hasaa baada ya kuchapishwa kwa kanda fulani za sauti.
Kampuni ya EMTEL, ambayo hutoa huduma za mawasiliano nchini humo, imethibitisha kuwa inatekeleza agizo hilo.