Mauaji ya George Thuo: Watuhumiwa wahukumiwa kifungo cha miaka 15 jela

Martin Mwanje
1 Min Read

Watuhumiwa wote sita wa mauaji ya aliyekuwa mbunge wa Juja George Thuo wamehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela. 

Hukumu hiyo itakayoanza kutumika Aprili 19, 2024 imetolewa leo Jumanne na Jaji Roselyn Korir katika mahakama ya Milimani.

Sita hao walipatikana na hatia ya kumuua Thuo Aprili 19, 2024.

Mbunge huyo wa zamani wa Juja aliuawa mnamo mwaka wa 2013 na  kesi dhidi ya sita hao imeendelea kwa kipindi cha miaka 12 sasa.

 

Website |  + posts
Share This Article