Waziri wa afya Susan Nakhumicha, amefichua kuwa bima mpya ya afya SHIF itaanza kutekelezwa mwezi Machi mwaka huu.
Waziri Nakhumicha alifichua hayo Alhamisi akiongeza kuwa wakaribia kukamilisha vipengee na sheria zinazoambatana na bima hiyo,kabla ya kuanza kutekelezwa rasmi.
Nakhumicha aliongeza kuwa bima hiyo itasimamia kila Mkenya huku wanaotaka huduma maaluma za matibabu, wakihitajika kulipia ada za zaidi kando.
Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini Waziri alisema kuwa matozo mapya ya bima hiyo, yataanza kukatwa kwenye mishahara ya wafanyikazi kuanzia mwezi Machi .