Matokeo ya KCSE: Watahiniwa 1,693 wapata Gredi ya A

Martin Mwanje
1 Min Read

Jumla ya watahiniwa 1,693 walipata Gredi ya A katika mtihani wa kidato cha nne wa KCSE uliofanywa mwaka jana. 

Kati ya gredi hizo, watahiniwa wa kike 556 walipata Gredi ya A ikilinganishwa na watahiniwa wa kiume 1,137.

Watahiniwa 7,743 walipata Gredi ya A- , 19,150 Gredi ya B+, 43,120 Gredi ya B, 75,347 Gredi ya B- huku watahiniwa 99,338 wakipata Gredi ya C+.

Watahiniwa 246,391 walifuzu kujiunga na vyuo vikuu baada ya kupata Gredi ya C+ na zaidi.

Hata hivyo, matokeo ya watahiniwa 840 yamefutiliwa mbali baada ya watahiniwa hao kujihusisha katika visa vya udanganyifu wakati wa kufanywa kwa mtihani huo.

Jumla ya watahiniwa 962,512 walifanya mtihani wa KCSE mwaka 2024.

Kati ya watahiniwa hao, 480,310 walikuwa wa kiume na 482,202 wa kike.

Hii ni mara ya kwanza kwa idadi ya watahiniwa wa kike kuzidi ile ya watahiniwa wa kiume nchini.

Watahiniwa wanaweza wakapata matokeo yao kwa kubonyeza linki ifuatayo: https://results.knec.ac.ke.

Watahiniwa watahitajika kuweka nambari na jina lao la usajili wa mtihani huo ili kupokea matokeo.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *