Matayarisho kwa makala ya nne ya mbio za kila mwaka za Sirikwa Classic World Cross Country Tour yameshika kasi.
Makala ya mwaka huu yataandaliwa Februari 22 Lobo Village eneo la Kapseret kaunti ya Uasin Gishu.
Waandalizi wamesema kuwa wanariadha watakuwa na changamoto mpya katika uwanja ikiwemo kunyunyuziwa maji watakapokimbia.
Mbio za mwaka huu zitashirikisha vitengo vya kilomita 10 kwa wanaume na wanawake na kilomita 6 kwa wasichana.
Washindi wa kilomita 10 watatuzwa shilingi 960,000; washindi wa medali za fedha watapata shilingi 800,000 huku watakaomaliza nafasi ya tatu wakituzwa shilingi 640,000.