Matabibu Baringo wazindua uhamasisho kuhusu afya ya akili

Tom Mathinji
1 Min Read
Matabibu Kaunti ya Baringo.

Huku ulimwengu unapojiandaa kuadhimisha siku ya kimataifa kuhusu afya ya akili mnamo tarehe 10 mwezi huu, kundi moja la wataaalam wa matibabu katika kaunti ya Baringo limeanzisha kampeni ya uhamasisho kuhusu matatizo ya kiakakili.

Wakizungumza katika hospitali ya kaunti ndogo ya Eldama Ravine wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya wiki moja, wataalam hao walihoji umuhimu wa kuwaamasisha wananchi kuhusu afya ya kiakili na changamoto zake.

Wakiongozwa na Dkt. Solomon Sirma, ambaye ni waziri wa afya wa kaunti hiyo wataalam hao walielezea wasiwasi kuhusu ukosefu wa maarifa kuhusu matatizo ya kiakili.

“Wakazi wengi hutatizika bila kujua, wakikosa ufahamu wa dalili za ugonjwa wa akili,” alisema Dkt. Sirma.

Walisema afya ya akili ni muhimu sawa na afya ya kawaida na hivyo haipaswi kuonekana kama aibu.

“Ni muhimu tuvunje unyanyapaa unaozingira ugonjwa wa akili, na kuwapa changamoto waathiriwa watafute usadidizi wa kimatibabu,” aliongeza Sirma.

Kwa maandalizi ya siku hiyo, idara ya afya kaunti ya Baringo, inajiandaa kuhamasisha umma kwa kutoa mafunzo kuhusu kutambua matatizo ya afya ya akili na mbinu zilizopo ya matibabu.

Maudhui ya siku ya kimataifa kuhusu afya ya akili mwaka huu ni uwepo wa afya nzuri ya kiakili na raslimali za kushinikiza afya bora ya kiakili.

Share This Article