Kocha wa Sofapaka, Robert Matano, ametangaza kuigura klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya soka humu nchini.
Matano alijiuzulu jana kabla ya klabu ya Fountain Gate FC, inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania bara kumzindua kuwa mkufunzi wao mpya.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 60, ameiacha Sofapaka ikiwa ya saba ligini kwa alama 21.
Ezekiel Akwana ametwikwa jukumu la kuwaongoza Batoto Ba Mungu kwa muda.