Mataifa saba ya afrika kupokea mkopo wa dola bilioni 1 kutoka IMF

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirika la IMF limetangaza kuwa mataifa saba ya Afrika yatapokea mikopo ya jumla ya dola za Kimarekani bilioni moja .

IMF imesema baada ya kutathmini upya uwezo na mikakati iliyowekwa na nchi hizo mwezi Oktoba ,saba kati ya nchi nane zilizotuma maombi ya mikopo zitapokea mikopo ya zaidi ya dola bilioni moja za Marekani.

Mataifa yaliyoidhinishwa ni Somalia ambayo itapokea dola milioni 100,Jamhuri ya Demokrasia ya Congo itakayopokea dola milioni 200 nukta 3,Rwanda dola milioni 262,Tanzania dola milioni 150,Gambia dola milioni 10 nukta 9,Comoros dola milioni 4 nukta 7 na Senegal dola milioni 276.

Website |  + posts
Share This Article