Masomo ya watoto mayatima yapigwa jeki Kilifi

Martin Mwanje
1 Min Read

Shirika moja lisilo la kiserikali limezindua mradi wa shule ya mayatima wa thamani ya yuro 300, 000 katika kaunti ya Kilifi utakaotumiwa kutoa masomo ya kidini na elimu ya msingi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa awamu ya kwanza ya majengo mawili yanayoweza kuwatoshea wanafunzi 100, Dr. Yauz Shahin kutoka shirika la Dr. Shahin Help Foundation la Ujerumani amesema mradi huo utakuwa wa kisasa na utasaidia vijana mayatima ambao hawajapata nafasi ya kusoma.

Mkurugenzi wa shirila la Holistic Educational Trust kutoka nchini Uturuki, Selchuk Turk amesema wana mipango ya kuongeza majengo mawili kama hayo.

Mbunge wa Kilifi Kaskasini Owen Baya ambaye alihudhuria uzinduzi huo aliwapongeza wahisani hao kwa kujitolea kuendeleza elimu na akawomba kujenga hospitali ya kisasa katika eneo hilo la Mtondia miaka ijayo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *