Masoko ya mifugo yamefungwa katika kaunti ya Pokot Magharibi ili kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa miguu na midomo na kuweka karantini.
Kama hatua ya kutahadhari kufuatia msambao wa ugonjwa huo, hatua hiyo itadhibiti kusogea kwa mifugo ili kuzuia ugonjwa huo kuenea katika maeneo mengine.
Masoko ya mifugo yaliyoathiriwa ni pamoja na Kishaunet, Chepareria, Cheptuya, Orolwo na Chepkobegh ambayo yamefungwa kwa muda.
Ugonjwa huo siku chache zilizopita uliripotiwa katika soko la Chepareria ambapo ng’ombe wawili walifariki.
Maeneo mengine yaliyoathiriwa ni Batei, Sebit ,Kanyarkwat,Sook na Sigor.
Gavana wa kaunti ya Pokot Magharibi Simon Kachapin anasema wameimarisha vita dhidi ya ugonjw huo kupitia utoaji chanjo na matibabu kwa mifugo walioambukizwa.
Aliongeza kuwa wamepata dozi 15,000 za dawa ili kuwachanja mifugo hao.