Mashirika ya wakulima Lugari yanufaika na mashine ya kukausha mipunga

Boniface Mutotsi
2 Min Read

Mashirika nane ya kijamii ya wakulima wa mipunga wa kaunti ndogo ya Lugari katika kaunti ya Kakamega, wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kupokea mashine inayotumia miyale ya jua kukausha mazao.

Mashirika hayo yanajumuisha; Koromait Nafaka Jasho ya wadi ya Chekalini, Baco CBO, Marakusi Mali Shambani, Muungano CBO ya wadi ya Lugari, Mulembe CBO, Mbagara Farmers ya wadi ya Mautuma, Lumakanda Maize Producers na Mercy CBO ya wadi ya Lumakanda.

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa kwa bidhaa hizo nje ya ofisi ya kilimo ya Lumakanda, afisa mkuu wa kilimo wa kaunti ndogo ya Lugari Kakai Wekesa, alishukuru mpango wa kuimarisha mpunga nchini kupitia Climate Resilient Agriculture Livelihoods.

Aliongeza kuwa, ‘’Lugari ni eneo la upanzi wa mahindi. Wakulima wamepata hasara wakati wa masika wanapovuna hivyo kukauka kwa mipunga huwa changamoto kuu.’’Alisema wekesa.

Aidha, aliwataka wakulima hao kutumia vyema mashine hizo.

Naye msambazaji wa mashine hizo Rodgers Alinda kutoka kampuni ya Sky Bold, alifichua kuwa mashine hizo zina uwezo wa kukausha kati ya kilo 500-600 kwa masaa mawili au matatu kutegemea kiwango cha unyevunyevu au miyale ya jua.
Kwa upande wao, katibu wa Lumakanda Maize producers –Soul Ombunge na Hudson Lomosi wa Koromait Nafaka jasho CBO, walipongeza mpango huo na kuhoji kuwa utawasadia pakubwa kuepuka hasara ya mara kwa mara.

Boniface Mutotsi
+ posts
Share This Article