Mashindano ya Riadha Ulimenguni yanukia Budapest, Hungary

Dismas Otuke
1 Min Read

Makala ya 19 ya mashindano ya kuwania ubingwa wa Riadha Ulimwenguni yataandaliwa mjini Budapest nchini Hungary kati ya Agosti 19 na 27 mwaka huu.

Jumla ya wanariadha 2,000 kutoka mataifa 202 watashindana katika fani 49 za riadha ndani ya kipindi cha siku 9.

Waanariadha 37 kati ya 44 walioshinda medali za dhahabu mwaka 2022 mjini Oregon nchini Marekani watakuwa wakitetea mataji yao mjini Budapest.

Kenya imetuma kikosi cha wanariadha 57 watakaoshiriki fani 18 tofauti huku Faith Kipyegon na Emanneuel Koriri wakiwa wanariadha pekee kutoka humu nchini wanaotetea mataji ya mwaka  jana mjini Oregon.

Kenya inaazimia kuboresha matokeo ya mwaka uliopita ilipozoa medali 10, dhahabu 2, fedha 5 na shaba 3.

Samuel Gathimba Ireri atakuwa mwanariadha wa kwanza kuwania medali kwa Kenya atakaposhiriki fainali ya matembezi kilomita 20 mapema Jumamosi katika siku ya kwanza

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *