Mashemeji waogopana kwenye derby ya Ligi Kuu Kenya

Ilikuwa sare ya 35 baina ya watani hao, matokeo yanayowaacha Gor katika nafasi ya tatu kwa pointi 43, kutokana na mechi 24, wakiwa pointi 5 nyuma ya vinara Police FC.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Kenya, Gor Mahia wameambulia sare tasa na AFC Leopards, katika derby ya 96 ya Mashemeji iliyochezwa leo jioni katika uwanja wa taifa wa Nyayo.

Timu zote zilicheza kwa umakini mkubwa huku zikibuni nafasi haba za kufunga mabao.

Ilikuwa sare ya 35 baina ya watani hao, matokeo yanayowaacha Gor katika nafasi ya tatu kwa pointi 43, kutokana na mechi 24, wakiwa pointi 5 nyuma ya vinara Police FC.

Ingwe nao wanasalia katika nafasi ya tano kwa alama 37, pointi 11 nyuma ya viongozi Police FC.

Kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa janga la Covid-19, mashabiki walifurika katika uwanja wa Nyayo kutazama derby hiyo.

Katika matokeo mengine, Shabana FC ikiwa nyumbani imeititiga Murang’a Seal mabao 3-0, Lastborn Aguero, akitisa nyavu mara mbili naye Ezekiah Omuri akiongeza moja .

Kakamega Homeboyz, wakiwa nyumbani, wametoka nyuma na kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya Kenya Commercial Bank, wakati Mohammed Bajaber, akipachika bao pekee na kuwapa Police FC ushindi dhidi ya Posta Rangers.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *