AFC Leopards itakuwa mwenyeji wa Gor Mahia katika derby nambari 94,ikiwa mechi ya ligi kuu nchini .
Gor wanakalia nafasi ya 3 kwa alama 8 kutokana na mechi 5, huku Ingwe wakishikilia nafasi ya 15 kwa alama 3 pekee.
Mara ya mwisho Mashemeji walipokutana mwezi Mei mwaka huu, Leopards waliibuka kidedea.
Katika mikutano ya awali Gor ukipenda Sirikal wanavunia kushinda mechi 31, wakati Chui wakishinda michuano 27 na 34 iliyosalia ikaishia sare.
Gor Mahia wameshinda mechi 9 kati ya 12 za hivi punde.
Mchuano wa Jumamosi utaanza saa kumi alasiri huku tiketi zikiuzwa kwa shilingi 1000 kwa zile za VVIP,shilingi 300 kwa VIP na 200 kwa maeneo ya kawaida.