Mashambulizi ya Israel huko Yemen yasababisha vifo 9

Kituo cha runinga cha Al Masirah kinachoendeshwa na wapiganaji wa Houthi wa Yemen kilitangaza kwamba watu saba waliuawa kwenye shambulizi la Israel katika bandari ya Salif.

Marion Bosire
2 Min Read
Jiji la Sanaa nchini Yemen

Mashambulizi kadhaa ya angani yaliyotekelezwa na Israel yalitikisa jiji kuu la Yemen na jiji la bandari na kusababisha vifo vya watu 9, kulingana na vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na wa-Houthi.

Jeshi la Israel lilisema lilishambulia vituo vya kijeshi vya wapiganaji wa Houthi katika pwani ya magharibi na ndani ya Yemen Alhamisi, baada ya kukatiza kombora lililorushwa na kundi hilo kuelekea Israel.

Kituo cha runinga cha Al Masirah kinachoendeshwa na wapiganaji wa Houthi wa Yemen kilitangaza kwamba watu saba waliuawa kwenye shambulizi la Israel katika bandari ya Salif.

Wengine waliuawa katika mashambulizi mawili katika kituo cha mafuta cha Ras Issa maeneo yote yakiwa katika mkoa wa Magharibi wa Hodeidah.

Kituo kingine cha habari cha SABA nchini Yemen kiliripoti mashambulizi manne yaliyolenga eneo la Hodeidah, huku mawili kati yao yakilenga kituo cha mafuta cha Ras Isa ambapo mtu mmoja alifariki na wafanyakazi wengine wakaachwa na majeraha.

Msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari alisema alifafanua kwamba wanajeshi wa Israel walishambulia vituo vya wapiganaji wa Houthi vinavyojumuisha bandari na muindomsingi ya kawi huko Sanaa.

Kulingana naye, hiyo ilikuwa hatua ya kulipiza kisasi kombora la Houthi lililorushwa kuelekea Israel usiku ambalo liliharibiwa na mashambulizi mengine ya miezi 14 iliyopita.

Hussain al-Bukhaiti, mchanganuzi wa masuala ya kisiasa anayependelea wapiganaji wa Houthi aliambia wanahabari kwamba Israel ilitekeleza mashambulizi 13 nchini Yemen Alhamisi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *