Mwanahabari Jacque Maribe ameondolewa mashtaka ya mauaji ya mfanyabiashara Monicah Kimani mtaani Kilimani mwaka 2018.
Kwenye hukumu iliyotolewa Ijumaa na jaji Grace Nzioka, kulikosekana ushahidi wa kutosha wa kumhusisha Maribe na mauaji ya marehemu Kimani.
Maribe ni mshatikiwa wa pili katika kesi hiyo ya mauji ambayo imedumu kwa kipindi cha miaka mitano ambapo alishtakiwa pamoja na Joseph Irungu maarufu Jowie kwa tuhuma za kutekeleza mauaji hayo.
Jaji Nzioka amempata Jowie na hatia ya mauaji akiongeza kuwa alikuwa na utaalaam wa kuua na pia alimfahamu fika marehemu kinyume cha alivyojitetea.
Mwili wa Monicah Kimani ulipatikana katika chumba chake huko Lamuria Gardens mtaani Kilimani.