Marekani yatangaza kuwa wanajeshi waasi wa Sudan Rapid Support Forces wametekeleza mauaji ya halaiki

Dismas Otuke
1 Min Read
Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Serikali ya Marekani imetangaza kuwa wanajeshi waasi wa Sudan’s Rapid Support Forces (RSF) wametekeleza mauaji ya halaiki kwenye mapigano ya raia yanayoendelea huku wanajeshi wa Sudan wakiwaua makumi ya maelfu na kusababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, amekashifu jeshi la RSF kwa kuwavamia raia,kutekeleza mauaji ya kikabila,kutekeleza dhulma za kingono na kuzuia uwasilishaji  wa misaada kwa raia .

Marekani imemwekea vikwazo kiongozi wa RSF Mohammad Hamdan Daglo Mousa, na washirika wenzake saba walio katika muungano wa Milki za Kiarabu.

Mzozo huo ulioanza April 2023 umesababisha mamilioni kutoroka makwao na kuchangia ukame na njaa katika baadhi ya maeneo ya Sudan.

Marekani imeapa kuwachukulia hatua za kisheria wote ambao wanahusika kwa mauaji ya raia .

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *