Serikali ya Marekani imemwekea vikwazo mkuu wa majeshi ya Sudan Abdel Fah Burhan.
Inamtuhumu kwa kuendeleza vita badala ya mashauriano.
Vita vya kijeshi nchini Sudan vimechangia vifo vya zaidi ya watu 10,000 huku mamilioni ya wengine wakihama makwao.
Marekani na Saudi Arabia zimejaribu bila mafanikio kutafuta suluhu ya kumaliza vita hivyo kwa kutumia majadiliano.