Marekani yajiandaa kuwaokoa raia wake kutoka Sudan

Tom Mathinji
1 Min Read

Marekani inajiandaa kupeleka wanajeshi zaidi kwenye kambi yake ya kijeshi nchini Djibouti kuisaidia iwapo watahitajika kuwaokoa raia wa taifa hilo kutoka nchi jirani inayokumbwa na vita ya Sudan.

Hatibu wa ikulu ya White House John Kirby, alisema rais wa Marekani Joe Biden aliagiza wanajeshi kuwekwa katika hali ya tahadhari huku akifuatilia matukio nchini Sudan.

Kirby hata hivyo amesema hakuna dalili  kwamba raia wa Marekani wanalengwa kwenye vita nchini  Sudan.

Djibouti, ambalo ni taifa dogo zaidi likiwa na takribani watu milioni moja limekuwa nguzo muhimu kwa operesheni za kijeshi za marekani barani afrika na mashariki ya kati.

Marekani ilifanikiwa kutia saini mkataba wa kukodi kambi hiyo ya kijeshi kwa kipindi cha miaka 10 mnamo mwaka wa 2014 na hulipa serikali ya Djibouti dola milioni 63 kila mwaka.

Vikosi vya wapiganaji vinavyoongozwa na viongozi waliounga mkono baraza la mpito linalotawala nchini Sudan vilianzisha vita mwishoni mwa juma lililopita kutafuta kuchukua mamlaka ya taifa hilo ambavyo vimesababisha vifo vya watu 330 kufikia sasa, na kuliweka taifa hilo katika hali mbaya ya kibinadamu, kulingana na umoja wa mataifa.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *