Marekani yaipa Kenya shilingi milioni 150 kukabiliana na athari za mafuriko

Tom Mathinji
1 Min Read

Kenya imepokea msaada wa shilingi milioni 150 kutoka serikali ya Marekani, kusaidia mikakati ya kukabiliana na athari za mafuriko.

Akizungumza wakati wa kuzindua msaada huo, balozi wa Marekani hapa nchini Meg Whitman, alisema shilingi milioni 38 zitapelekwa moja Kwa moja katika shirika la msalaba mwekund, ambalo lilipokea chakula zaidi cha msaada na vifaa vingine kutoka shirika la Marekani la maendeleo ya  Kimataifa USAID.

Kulingana na hatibu wa serikali Isaac Mwaura, watu  174 wepoteza maisha kutokana na mvua kubwa inayoshuhudiwa katika baadhi ya sehemu za hapa nchini

Kulingana na Mwaura, watu sita zaidi waliofariki katika muda wa siku tatu zilizopita kutoka na mafuriko.

Sita hao ni pamoja na mama na mtoto kutoka Kijiji cha Ngurunga, kaunti ya Kiambu,na wachimba migodi wanne katika kaunti ya Migori.

Mwaura alidokeza kuwa mvua kubwa ilinyesha kaunti ya Kitui siku ya Jumatatu na kusababisha uharibufu mkubwa wa barabara na kuwaua mbuzi 56.

“Tumeweka kambi zaidi za kuwahifadhi waathiriwa wa mafuriko, huku idadi ya kambi hizo ikiongezeka hadi 170 kote nchini,” alisema Mwaura.

Share This Article