Marekani na Iran zakubaliana kusitisha mapigano

radiotaifa
1 Min Read
Iran na Marekani zakubaliana kusitisha mapigano.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema Marekani na Iran zimekubaliana kukomesha mapigano kwa muda wa wiki mbili.

Akihojiwa na shirika laAgence France , Trump alisema Katika kipindi hicho, mlango wa bahari wa Hormuz utafunguliwa kutoa fursa kwa meli kupita.

Haya yanajiri huku Iran ikitoa masharti yake ya kusitisha mapigano hayo yenye vigezo 10, ikiwa ni pamoja na kuratibiwa kwa majeshi ya Iran kudhibiti shughuli za usafirishaji bidhaa katika kiingilio cha Hormuz, kukomeshwa kwa uhasama dhidi ya washirika wake, na kuondolewa kwa vikosi vya Marekani katika kambi za eneo hilo.

Hatua ya kusitishwa mapigano kati ya Marekani na Iran ilitangazwa yapata dakika 90 kabla ya kukamilika kwa makataa ya rais Trump kwa Iran kuafikia makubaliano.

Pakistan, ambayo imekuwa mpatanishi kwenye mazungumzo hayo, imealika pande zote mbili kwa mazungumzo huko Islamabad Ijumaa, huku waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer akielekea eneo la ghuba kutafuta usaidizi wa kusitisha mapigano hayo.

Share This Article