Marekani kufutilia mbali Viza za raia wa Sudan Kusini kwa ukaidi

Sudan Kusini, inakabiliwa na utovu wa usalama huku Rais Riek Machar, akiwekwa chini ya kifungo cha nyumbani wiki iliyopita.

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali ya Marekani imeapa kufutilia mbali viza zote za usafiri zinazomilikiwa na raia wa Sudan Kusini kutokana na kile ambacho imekitaja kuwa ukaidi.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio, ameikashifu Sudan Kusini, kwa kukataa kuwakubali raia wake waliofurushwa majuzi kutoka nchini Marekani.

Aidha, Rubio amesema kuwa watazuia maombi yote mapya ya viza kutoka kwa raia wa Sudan Kusini, wanaotaka kuingia Marekani.

Rais mstaafu wa Marekani Joe Biden, alikuwa amewapa kibali cha muda raia wa Sudan Kusini, kibali ambacho muda wake unakamilika tarehe 3 mwezi ujao.

Kibali hicho hupewa kwa watu ambao wanakumbwa na vita katika mataifa yao.

Hata hivyo, wengi wanahofia kuwa kurejeshwa kwa raia hao nchini Sudan Kusini, huenda kukasababisha vita vibaya zaidi kwa raia kuwahi kutokea.

Sudan inakabiliwa na utovu wa usalama huku Rais Riek Machar, akiwekwa chini ya kifungo cha nyumbani wiki iliyopita.

Serikali ya Rais Donald Trump, imeapa kuwarejesha makwao raia wote wa kigeni walio nchini humo bila vibali, hali ambayo imezua mtafaruku.

Website |  + posts
Share This Article