Tanzania yaondoa amri ya kutotoka nje usiku

Tom Mathinji and BBC
1 Min Read
Serikali ya Tanzania yaondoa amri ya kutotoka nje usiku.

Huku hali ya kawaida ikiendelea kurejea nchini Tanzania baada ya maandano wakati wa Uchaguzi Mkuu, serikali ya nchi hiyo imeondoa amri ya kutotoka nje usiku.

Polisi kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki, walitangaza amri ya kutotoka nje kuanzia saa kumi na mbili jioni, kutokana na ghasia zilizoghubika baadhi ya sehemu za nchini hiyo wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Vile vile serikali meondoa vikwazo vya usafiri na huduma za internet kurejeshwa na kusababisha wananchi wa kuendelea na shughuli zao za kawaida.

Milango ya vituo vingo vya kibiashara ilifunguliwa, ambayo ilifungwa kutokana na ghasia hizo.

Siku ya Jumanne, serikali ya Tanzania ilitoa taarifa kwa wafanyakazi wote kurejea katika shughuli zao kama kawaida.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article