Marehemu Kiptum kuzikwa Ijumaa, mazishi kuongozwa na Rais Ruto

Dismas Otuke
1 Min Read

Mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon Kelvin Kiptum atazikwa Ijumaa nyumbani kwake kijijini Naiberi  kaunti ya Uasin Gishu.

Mazishi hayo yanatarajiwakuongozwa na Rais William Ruto na viongozi wengine wakuu serikalini.

Maelfu ya waombolezaji wakiongozwa na wanariadha waliongoza msafara wa kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka makafani ya Eldoret na pia shughuli ya kuutazama mwili kwa umma iliyoandaliwa karibu na nyumbani .

Kiptum aliye na umri wa miaka 24 alifariki Feberuari 11, katika ajali ya barabarani pamoja na kocha wake Gervais Hakizimana aliyezikwa juzi

Mwanariadha huyo ambaye alikuwa amejumuishwa katika kikosi cha Kenya cha Olimpiki mwaka huu  alitwaa ubingwa wa London Marathon mwaka jana, kabla ya kushinda mbio za Chicago Marathon huku akiandikisha rekodi mpya ya dunia ya saa 2 na sekunde 35.

Mola ailaze roho yake mahala pema.

Share This Article