Rais wa Comoros Azali Assoumani na mwenzake wa Jmahuri ya Afrika ya Kayti Faustin Archange Touadera, wamewasili Nairobi Jumapili tayari kwa kongamano la kimataifa la Marais wa Afrika, IDA21 litakaloandaliwa Jumatutu katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano KICC.
Kongamano hilo la kiuchumi linaandaliwa na Benki ya Dunia na linajiri wakati mataifa mengi ya Afrika yanakabiliwa na changamoto ya kifedha za aidha kufufua uchumi au kustawisha uchumi.
International Development Association(IDA) hutoa asilimia 70 ya mikopo nafuu kwa mataifa wanachama wa Benki ya Dunia na pia ruzuku ,kuyawazesha mataifa kuwekeza katika miradi ya kuinua jamii.