Wakulima wa kahawa katika kaunti ya Nyeri watapata fursa ya kutangamana na wanunuzi wa kahawa yao moja kwa moja wakati wa maonyesho ya kilimo ya kahawa yatakayofanyika kwa kipindi cha siku saba mwezi ujao.
Hii ni baada ya muungano wa maonyesho ya kahawa kutia sahihi mkataba na serikali ya kaunti hiyo kufanikisha maonyesho hayo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Gavana wa kaunti ya Nyeri Mutahi Kahiga ameyataka mashirika ya kahawa katika kaunti hiyo kufanya maonyesho ya kufana ili wawekezaji wanunue kahawa yao moja kwa moja badala ya kutumia mawakala.
Kaunti ya nyeri ni mojawapo ya kaunti ambazo huvunwa kahawa iliyo na ubora kiwango cha juu zaidi nchini.