Bondia Karim Mandonga aka mtu kazi, amefungiwa kushiriki mashindanoni na tume ya kudhibiti ngumi za kulipwa nchini Tanzania TPBRC kwa hofu ya kuwa na matatizo ya kia akili.
‘Mtu Kazi’ amezuiwa kushiriki mapigano yoyote akisubiri ripoti ya utathmini wa afya yake kutoka hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Tume ya TPBRC imeagiza kuchunguzwa kwa afya ya mwanamasumbwi huyo ambaye ameshiriki mapigano 9 katika kipindi cha miezi 11 iliyopita na alipangiwa kushuka ulingoni kwa pigano jingine nchini Zanzibar tarehe 27 mwezi huu.
Mandonga alishiriki mapigano 4 ndani ya siku 35 ikiwemo kupigwa na Moses Golola wa Uganda Julai 29, alipopigwa kwa Knock Out wiki moja baada ya kushinda na Daniel Wanyonyi wa Kenya jijini Nairobi
Kulingana na Katibu Mkuu wa tume ya TPBRC George Lukindo, Mandonga atafanyiwa vipimo vya MRI baada ya kushindwa kupitia Knock Out na Golola.
Mandonga ameshinda mapigano 6, kupoteza matatu na kwenda sare mapigano mawili.