Mancity watwaa ubingwa wa EPL mara nne kwa mpigo

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya Manchester City imehifadhi ligi kuu nchini Uingereza kwa mara ya nne mtawalia, baada ya Kuizaba West Ham mabao matatu Kwa moja kwenye mechi ya kufunga msimu wa 2023/ 2024.

Mabao mawili ya mwanzo ya City yalitiwa kimiani na Fill Foden dakika ya pili na 18.

West Ham waliimarika na kupata bao kupitia Mohammed Kudus kipindi cha kwanza kikiishia kwa uongozi wa City wa 2-1.

Hata hivyo, Rodri alifungia City la tatu dakika ya 59 na kuzamisha matumaini ya West Ham.

Mancity ndio timu ya kwanza kutwaa taji ya Ligi kuu uingereza mara nne kwa mpigo.

Ushindi huu ni wa alama 91 wakifuatwa na Arsenal Kwa alama 89. Liverpool na Aston Villa wanafunga nne Bora Kwa alama 82 na 68 mtawalia.

Share This Article