Mabingwa watetezi wa taji ya Ligi ya Mabingwa barani ulaya Manchester City watamenyana tena na Real Madrid ya Uhispania katika robo fainali mwezi ujao.
Timu hizo zilikumbana msimu uliopita Mancity wakiibandua Madrid kwa ushindi wa jumla,wa mabao 4-1 katika nusu fainali.
Mkondo wa kwanza wa robo fainali utaandaliwa ugani Santiago Barnabeu April 9 huku marudio yapigwe tarehe 16 April kiwarani Etihad.
Katika droo nyingine ya kwota fainali Arsenal wataanzania nyumbani dhidi ya mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich, huku Borusia Dortmund wakianzia ugenini dhidi ya Atletico Madrid.
PSG ya ufaransa watamaliza udhia nyumbani dhidi ya Barcelona.
Mshindi kati ya Munich na Arsenal atacheza nusu fainali na mshindi baina ya Mancity na Madrid, huku mshindi kati ya PSG na Barcelona akiwa na miadi ya nusu fainali dhidi atakayeshinda baina ya Atletico na Dortmund.
Nusu fainali zimeratibiwa kuchezwa baina ya April 30 na Mei 7 kwa mkondo wa kwanza na wa pili mtawalia.
Fainali itasakatwa Juni Mosi katika uchanjaa wa Wembley nchini Uingereza