Manchester United yamnyatia Amrabat

Dismas Otuke
1 Min Read

Manchester United wamejitosa kwenye kinyang’anyiro cha kiungo mkabaji wa Fiorentina Sofyan Amrabat wa Morocco.

Amrabat aliye na umri wa miaka 26 anapania kukata tamaa na Atletico Madrid ambao wanawinda huduma zake katika msimu wa sasa wa uhamisho.

Yamkini meneja wa Madrid Diego Simeone anapania kumsajili Pierre-Emile Hojbjerg wa Tottenham badala ya Amrabat.

Amrabat alisakata mechi 34 za serie A msimu uliopita na pia alitia fora katika fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar akiwa na Atlas Lions.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *