Matumaini ya klabu ya Manchester United kufuzu kwa raundi ya mwondoano kuwania ligi ya mabingwa yalianza kudidimia, baada ya kuambulia kichapo cha magoli manne kwa matatu ugenini Denmark dhidi ya Copenhagen.
Marcus Rushford ilipigwa kadi ya umeme kunako dakika ya 42 ya mchezo, Man U wakiongoza mabao mawili kwa bila na mechi ikageuka kipindi cha na wenyeji wakasajili ushindi wa kihistoria.
Man U ni ya mwisho katika kundi A kwa pointi 3 baada ya mechi nne ,alama 1 nyuma ya Galatasaray na Copenhagen na ni sharti washinde mechi mbili za mwisho ili kuwa na nafasi ya kufuzu kwa raundi ya 16 bora.