Klabu ya Manchester City ndio mabingwa wa kombe la dunia kwa mara ya kwanza, baada ya kuwazabua Fluminense FC ya Brazil, magoli manne bila jibu kwenye fainali ya Ijumaa usiku katika uwanja wa King Abdallah Sports nchini Saudi Arabia.
Julián Álvarez alifungua karamu ya magoli kwa mabingwa wa ulaya kwa bao la dakika ya kwanza, kabla ya Fluminense kujifunga la pili dakika ya 27 kupitia kwa Nino.
Phil Foden alitanua uongozi kwa la tatu dakika ya 72, akiunganisha pasi ya Alvarez na kisha Alvarez akafunga ukurasa kwa bao la nne dakika ya 88, baada ya kuunganisha pasi ya Mathews Nunes.
Mabingwa wa Copa Libertadores Fluminense waliondoka uwanjani baada ya dakika 90 wakiwa na mafunzo tosha wakiridhia nishani ya fedha.
City ndiyo timu ya kwanza ya Uingereza kutwaa mataji yote manne,ligi kuu Uingereza,livi ya mabingwa ulaya,UEFA Super na kombe la Dunia.