Mamlaka ya KURA kufunga barabara ya Limuru-Aga Khan Agosti 20 kupisha ukarabati

Dismas Otuke
1 Min Read

Mamlaka ya usimamizi wa barabara za mijini nchini (KURA), imetangaza kutatizika kwa usafari kwenye barabara ya Limuru, na Aga Khan Primary Jumapili hii Agosti 20 kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa mbili jioni.

Kulingana na arifa ya KURA, wakandarasi watakuwa wakibomoa kivuko kilichowekwa eneo hilo kwa matumizi wa ya watu wanaotembea ili kuipanua barabara hiyo na kuwa na safu mbili za kusafiria.

Mamlaka ya KURA imetawaka waendeshaji magari kuwa makini siku ya Jumapili wakikaribia eneo hilo na waelekezaji watakuwepo kuwaongoza madereva.

Website |  + posts
Share This Article