Mamia ya raia wa Morocco wakamatwa wakitorokea Uhispania

Dismas Otuke
1 Min Read

Mamia ya raia wa Morocco walikamatwa na maafisa wa polisi siku ya Jumapili wakijaribu kutorokea nchini Uhispania, kwa kuogelea katika ufukwe wa Ceuta ulio mpakani mwa nchi hizo mbili.

Kulingana na maafisa wa polisi watu hao walitumia fursa ya ukungu uliotanda na kuogelea kuvuka bahari ya Mediterenean siku ya Jumapili.

Morocco na Uhispania zinatenganishwa na bahari ya Mediterenea huku idadi kubwa wahamiaji wa kutoka Afrika ikiripotiwa kujaribu kuvuka mpaka, kupitia taifa hilo la kaskazini kuingia Ulaya.

.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article