Mamia wauawa Sudan kutokana na vita baina ya jeshi na RSF

Dismas Otuke
1 Min Read

Mji wa Darfur na viunga vyake nchini Sudan ulizagaa miili ya watu waliouawa jana Alhamisi kufuatia makabiliano kati ya vikosi viwili vya jeshi.

Jeshi linalomuunga mkono Abdel Fettah al-Burhani, limekuwa likipigana na kundi lenye hadhi ya kijeshi la Rapid Support Forces, RSF linaloongozwa na Mohammed Hamdan Daglo tangu Aprili 15 mwaka huu.

RSF imekuwa ikidai kutawala mji wa Dafur ambao unapiganiwa na pande zote.

Watu zaidi ya 10,000 wameuawa tangu kuanza kwa vita hivyo na kuwalazimu maelfu ya raia kuhama kutokana na ukosefu wa usalama na kukatizwa kwa umeme.

Share This Article