Azma ya vipusa wa Kenya-Malkia Strikers kujiakatia tiketi kwa nusu fainali ya mashindano ya Challenger Cup nchini Ufilipino, imezimwa baada ya kutitigwa seti 3-0 (20-25, 19-25, 25-27) siku ya Alhamisi na Puerto Rico.
Mchuano huo ulikuwa wa kwanza kwa Kenya katika mashindano hayo.
Malkia Strikers wanaofunzwa na kocha mkuu Japheth Munala, watarajea uwanjani Ijummaa dhidi ya The Galeries Tower Highrisers ya Ufilipino ambayo yatakuwa matayarisho ya mwisho Ijumaa,kabla ya kuanza kwa michezo ya Olimpiki Paris,France.
Kenya imejumuishwa kundi B katika makala ya 31 ya michezo ya Olimpiki ya mwaka huu na watafungua ratiba dhidi ya Brazil Julai 29 kabla, ya kukabiliana na Poland tarehe 31 na kuhitimisha ratiba dhidi ya Japan terehe Agosti 3.